KUCHUNGA NG'OMBE HADI WAZIRI MKUU _

ROBY MEDIA
0

KUCHUNGA NG'OMBE HADI WAZIRI MKUU


_

 KUCHUNGA NG'OMBE HADI WAZIRI MKUU

_

Mwigulu Nchemba, mwenye umri wa miaka 50, ndiye Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi wake umetangazwa rasmi bungeni Dodoma na kuthibitishwa kwa kura 369 za ndiyo kati ya 371, ishara tosha ya imani kubwa kwake.


Ni mwana wa Singida, aliyekulia kijijini na kupitia maisha magumu ya ufugaji na umaskini, lakini leo hii anasimama kama kiongozi wa serikali.



“Mimi umasikini wa Tanzania sijausoma kwenye kitabu — nimeuishi.”- Alisema Nchemba kwa hisia baada ya kuthibitishwa.


Anasema maisha ya kuchunga ng’ombe na nyumba zinazovuja ndiyo yaliyomjenga kuwa na nidhamu, uvumilivu na moyo wa kutumikia wananchi.


📚 Alisoma:-

➡️ Shule ya Msingi Makunda (1987–1993)

➡️ Sekondari Ilboru na Mazengo

➡️ Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Shahada ya Uchumi, Uzamili (2006) na Uzamivu 🎓


Leo anakuwa mfano wa kijana wa Kitanzania aliyepanda ngazi kwa jasho, si kwa bahati. 🌟


👉 Kamwe usidharau mwanzo wako.

👉 Kile unachopitia leo kinaweza kuwa ushuhuda wako kesho.


#MwiguluNchemba #WaziriMkuuMpya #Tanzania #Dodoma #SingidaPride #Leadership #Inspiration #TanzaniaUpdates

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default