LIST NZIMA YA WASHINDI WA TUZO ZA CAF 2025
✅Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco na PSG Achraf Hakimi ndiye MVP wa Afrika akiwasginda Mo Salah na Osimhen
✅Mshambuliaji wa Pyramids na timu ya taifa ya DR Congo, Fiston Kalala Mayele ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2025 barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya bara la Afrika.
Kumbuka ndio straika aliyefunga magoli mengi kwenye msimu uliopita wa CAF Champions League, magoli 6
✅Golikipa wa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia na timu ya taifa ya Morocco Yassine Bounou ametwaa tuzo ya Golikipa bora mwaka 2025 barani Afrika
✅Klabu ya Pyramids kutoka Misri imetwaa tuzo ya klabu bora ya mwaka 2025 barani Afrika kuwashinda:
RS Berkane (Morocco)
Mamelodi Sundowns (South Africa)
Kumbuka Pyramids ndio mabingwa wa CAF Champions League na CAF Super Cup 2025
✅Timu ya taifa ya Morocco chini ya umri wa miaka 20 imetwaa tuzo ya timu bora ya taifa ya mwaka 2025 kwa upande wa wanaume barani Afrika
Kumbuka Morocco U20 wametoka kutwaa kombe la Dunia 2025 baada ya kuitungua Argentina U20, 2-0 katika mchezo wa fainali.
✅Mshambuliaji wa klabu ya Watford ya England na timu ya taifa ya vijana ya Morocco, Othmane Maamma ametwaa tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka 2025 barani Afrika
✅Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Clement Mzize ametwaa tuzo ya goli bora la mwaka 2025 barani Afrika.
Mkwaju wa mbali ambao alimtungua golikipa wa klabu ya TP Mazembe.
✅Kocha wa timu ya taifa ya Cape Verde, BUBISTA ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka 2025 barani Afrika
Kumbuka Bubista ameiongoza Cape Verde kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani kwa mara ya kwanza katika Historia ya taifa hilo lenye raia wachache sana.
✅Golikipa Bora wa mashindano upande wa wanawake Chiamaka Nnadozie wa Nigeria anachukua TUZO mara 3 mfululizo
✅ Doha El Madan wa Morocco ndiye Mchezaji Bora chipukizi wanawake
✅Othmane Maamma wa Morocco ndiye mchezaji Bora chipukizi wanaume
✅ Nigeria imeshinda TUZO ya timu Bora ya mwaka Kwa Wanawake


