MAMA WA HAMISA MOBETTO AFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA – UMRI WAZUA MASWALI, ASHUKIWA KUVUKA MIAKA 40

ROBY MEDIA
0

 MAMA WA HAMISA MOBETTO AFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA – UMRI WAZUA MASWALI, ASHUKIWA KUVUKA MIAKA 40



Mama mzazi wa mrembo na mfanyabiashara Hamisa Mobetto ameendelea kutawala vichwa vya habari baada ya kuonekana akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa bashasha na tabasamu jepi lililovutia mitandao ya kijamii. Mama huyo, anayefahamika kwa jina lake halisi Shufaa Lutenga, ametumiwa salamu nyingi za pongezi na mashabiki, huku wengi wakimpongeza kwa kuonekana mwenye afya njema na sura changa licha ya kukadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 40.
Shufaa Lutenga, ambaye ni msukuma halisi, ameonekana kuvuta hisia za watu wengi kutokana na upekee wa jina lake—majina ambayo, kwa wenyeji wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya Kanda ya Ziwa, ni ya kawaida na yenye historia ndefu katika ukoo wa Wasukuma. Mashabiki wengi wameonyesha kufurahia kuona upande wa familia ya Hamisa ambao mara nyingi hauonekani sana kwenye mitandao.
Katika mitandao mbalimbali, mashabiki wamemiminika kumtakia mama huyo maisha marefu, afya tele na baraka zaidi, huku wengine wakimpongeza kwa kulea staa mkubwa kama Hamisa Mobetto ambaye amekuwa mfano wa mwanamke mwenye juhudi kwenye tasnia ya burudani, urembo na biashara.
Sherehe hizo zimeonyesha kwa mara nyingine namna familia ya Mobetto inavyoenzi umoja na upendo, huku msimu huu wa sikukuu ukiongeza mvuto zaidi katika tukio hilo maalum.
ROBYMEDIA itakupa updates zaidi pindi taarifa mpya zitakapofika mezani.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default