JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA
lipo Msumbiji lina miaka mitatu sasa nalo likipambana na Waasi na waliingia kwa Mwamvuli wa SADC kupitia Oparesheni ya SAMIM ambapo baada ya Mission hiyo kutamatika Jeshi letu bado limesalia kule kuhakikisha wanaendelea kuwasogeza mbali Waasi huku wakishika Viteule vingi mpaka hivi sasa maana Kaskazini mwa Msumbiji ndio Kusini mwa Tanzania hivyo ni eneo la Kimkakati mno kwa Ulinzi wa Tanzania, ikumbukwe Majeshi mengine yote katika Oparesheni ile wameshaondoka ila sio JWTZ.
JWTZ wanasambaza njugu kuanzia eneo la Nangade huko Msumbiji ambapo ni karibu na Mto Ruvuma ambao ni Mpaka wa nchi hizo mbili huku Oparesheni hiyo ikitambulika kama KOBOKO ni OP ngumu mno ya Kijeshi Kusini mwa Afrika na vyombo mbalimbali vya Kimataifa vinalisifu mno Jeshi la Wananchi wa Tanzania haswa kwenye mapambano ya ardhini kupitia Special Forces na mara zote ISM wakijichanganya huwa wanachakaa vibaya sana ni Jeshi linaloogopeka mno na Mission imesukwa kwa Ustadi mno.
Kama hivyo haitoshi JWTZ wana Oparesheni nyingine muhimu OP MAMBA ambayo inatekelezwa ndani ya mipaka ya Tanzania huko Kusini katika kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Wananchi wa Tanzania, ambapo pia Wanajeshi wa Msumbiji wamevuka kuja Tanzania kusomeshwa Kijeshi ili kurudi kuendelea kupambania nchi yao.
📌📌

