📍ROBY MEDIA SPORTS UPDATE*
*📅 November 23, 2025*
*KARATA ZA PATEV ZAGOMA LEO MBELE YA WAANGOLA!*
Kocha Patev wa Simba SC aliingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa leo akiwa na matumaini makubwa ya kuendeleza ubabe wa nyumbani, lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo. Mbinu zake za leo hazikufua dafu mbele ya Waangola waliokuja kivingine kabisa.
Mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi na mapema, wakiamini timu yao ingeandika historia nyingine ya ushindi. Lakini kadri dakika zilivyoendelea kusogea, hali ya hewa ilianza kubadilika — mashambulizi ya Waangola yalionekana kuyumbisha kabisa safu ya ulinzi ya Simba.
Pamoja na juhudi binafsi za baadhi ya wachezaji wa Simba, mipango ya Patev haikuleta matokeo yaliyotarajiwa. Bao moja lililopachikwa na Waangola dakika za pili za kipindi cha pili lilitosha kuzima furaha ya mashabiki wa Msimbazi.
*Mashabiki wengi walionekana kukata tamaa, wengine wakiamua kuondoka uwanjani kabla ya mpira kumalizika.* Picha zao zikiangalia kwa huzuni kutoka jukwaani zinaeleza yote — karata za Patev leo zimegoma kabisa.
*Kocha Patev sasa anazidi kuwa kwenye presha kubwa, huku mashabiki na wadau wa klabu wakitaka majibu.*
—
*📌 Fuatilia updates zaidi kupitia:*
➡️ @ROBYMEDIA
📲 Facebook | Instagram | YouTube | Blog
#RobyMediaUpdates #SimbaSC #MkapaLive #FootballTZ

