Polisi Dodoma "Mtumba police station" inasemeka ndipo alipo Mch. Martini james.
John Heche Akiwasiliana na Mch. Mbarikiwa mwakipesile kuhusu taarifa za Mch. Martin James aliyepotea tokea tar 21 Oct 2025 alisema
"Mimi nilifungwa cello ya pekayangu, lakini nilisikia sauti ya mtu akiomba kwa sauti muda mwingi, na walikua wanamuita mchungaji, bila shaka ni yeye, nendeni mkamuangalie".
Pamoja na maelezo ya Mh. John heche, yupo shuhuda ambaye alifungwa pamoja na Mch. Martin James (Pichani) ndiye aliyeanza kutoa taarifa hizo kupitia namba za huduma za kikosi kazi cha injili.
Alisema, "Mchungaji yupo kituo cha polisi mtumba dodoma, aliniambia kama nitafanikiwa kutoka, naomba kawaambie ndugu zangu kwamba nipo hapa, namba utazipata kwenye channel ya YouTube ya kikosi kazi cha injili, wao watajua wanisaidiaje".
Kwa shuhuda za hao tunamini ni wazi kabisa kwamba jeshi la polisi linamshikilia mch. Martin James.
swali tunalojiuliza kwa nini wamshikilie bila kuwajuliza watanzania na waumini wa Mchungaji mpaka tunaumia bila matumaini?
Rai yetu ni kwamba Mch Martini James awe salama, kwani ni haki yake. ni vema polisi wamuachie huru, au waruhusu ndugu kumuwekea dhamana maana hana hatia.
MUNGU ATALIPA KILA MTU SAWA NA ATENDAYO.
Ameeeen

