Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo akizungumza na Wazee wa Dar es salaam, amesema kilichotokea October 29 2025 hakikuwa maandamano bali ni vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalum hivyo nguvu iliyotumika kuyadhibiti inaendana na tukio husika.

ROBY MEDIA
0

 Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo akizungumza na Wazee wa Dar es salaam, amesema kilichotokea October 29 2025 hakikuwa maandamano bali ni vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalum hivyo nguvu iliyotumika kuyadhibiti inaendana na tukio husika.



“Takwimu zinatolewa sasa hivi, kuna majengo kadhaa ya Serikali yameunguzwa, kuna miradi kadhaa iliyojengwa kwa maslahi ya Wananchi imeunguzwa, Vituo vya mafuta, biashara binafsi za Watu, magari ya Serikali, vituo vya Polisi vingi tu vimeunguzwa, sasa nataka tuwe na jina la hayo ni maandamano au vurugu? maandamano tuliyoyazoea na kuyakubali ndani ya Katiba ni yale Watu wameudhika na kitu tunaomba tuandamane tueleze tutatoka point moja hadi Mnazimmoja au popote pengine na mabango yanaeleza maudhi yetu na Polisi wanawasindikiza vizuri hadi wanapofika”



“Haya ya kuunguza miradi ya Serikali, vituo vya Polisi na kwenye kituo cha Polisi unakwenda kufanya nini? ni kwenda kuvamia na wapate silaha, madhumuni ya kuwa na silaha mkononi ni nini? haya hayakuwa maandamano zilikuwa vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalum”


“Serikali inawajibu tunaapa kuilinda mipaka ya Nchi hii na kulinda Raia na mali zao, katika hali hiyo nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo, sasa tunapoambiwa tulitumia nguvu kubwa sana kwenye tukio lile... nguvu ndogo ilikuwa ni ipi?, ilikuwa tuwangalie Waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi mpaka wafanikiwe? hapo patakuwa pana Dola kweli? Dola haipo hivyo"


"Na sio Tanzania tu hata Mataifa mengine Watu wakiandamana wanaweka nguvu kubwa, sasa wanapokuja kutulamu mlitumia nguvu kubwa wao walitaka nini?, tujiulize je hawa ndio Wafadhali wa kile kilichofanyika? walitaka tuangalie ile mob hadi ifanikiwe walichowapa fedha, walichowatuma? hapana” tuliapa kulinda Nchi hii na mipaka yake , usalama wa Raia na mali zao kwahiyo kama wanavyofanya wao na sisi tutafanya vilevile kuilindi Nchi yetu" - Rais Samia akiongea leo na Wazee wa Dar es salaam. #MillardAyoUPDATES

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default